Duration 1:35:58

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA : IBADA YA EVENING 27 / 12 / 2021

3 843 watched
0
69
Published 27 Dec 2021

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA : IBADA YA EVENING GLORY THE SCHOOL OF HEALING UJUMBE WA LEO 27 / 12 / 2021 : FAIDA ZA UPAKO WA ZERUBABELI JUU YA MTU KWA AJILI MIPANGO ALIYONAYO. NENO KUU : Zekaria 4:9 Mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na mikono yake ndiyo itakayoimaliza; nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwenu. Mwanzo 2 : 2 -3 Ayubu 22 : 28 Mwanzo 1 : 11 Isaya 46 : 10 Ufunuo 21 : 6 Ufunuo 21 : 3 - 6 Mwanzo 2 : 2 -3 2 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. 3 Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya. Ayubu 22 : 28 28 Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako. Mwanzo 1 : 11 11 Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo. Isaya 46 : 10 10 nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote. Ufunuo 21 : 6 6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure. Ufunuo 21 : 3 - 6 3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.b 4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. 5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli. 6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure. Mwl.George Mwakabago Mch. Dkt. Eliona Kimaro. Simu :+255655516053, +255754516053 YouTube : Rev. Dr. Eliona Kimaro TV Barua Pepe: elionakimaro555@gmail.com

Category

Show more

Comments - 6