Duration 25:35

TUNAPATA MAGONJWA YA HOVYO | WANANCHI WAKILALAMIKIA KIWANDA CHA DIZELI MVUTI ILALA

707 watched
0
8
Published 18 Nov 2021

Wananchi wa kijiji cha Kiboga, kata ya Msongola, wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam wameendelea kulalamikia kiwanda cha Guoyang Biotech Company Limited wanachodai shughuli zake zinaharibu mazingira na kuathiri afya zao pia. Kiwanda hicho kinachomilikiwa na raia wenye asili ya Kichina kilichopo kwenye kijiji cha Kiboga kinazalisha dizeli kwa ajili ya matumizi ya viwandani. Wakiongea na The Chanzo iliyofika kijijini hapo mnamo Novemba 8, 2021, kufuatilia kadhia hiyo, wananchi wa kijiji hicho walilamika kwamba kiwanda hicho kinatoa moshi mkali na harufu kali, vitu vinavyowafanya kukohoa sana, kutokwa na damu puani, kuzimia, na kutapika pia. Hata hivyo, mmoja kati ya watu wanaohusika na usimamizi wa kiwanda hicho Liu Xi Shung amesema moshi na harufu inayotoka kwenye kiwanda hicho ni ya kawaida, akitolea mfano kitendo cha wafanyakazi wake kutokuvaa barakoa kama ushahidi wa anachokisema. Shung anasema kwamba kuna siku moja tu kulitokea kasoro kwenye kiwanda hicho na kuzalisha moshi mwingi lakini hali hiyo haijajirudia tena.

Category

Show more

Comments - 3