Mbunge wa Momba David Silinde ni kati ya Wabunge waliosimama Bungeni leo kuchangia mapendekezo katika makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 ambapo amesema kama Serikali inahitaji kujenga uchumi na kuwasaidia wananchi wake ni lazima iwekeze katika zekta binafsi na sio kama inavyofanya sasa kwa kuzikandamiza.