Duration 14:32

Balile: Tangu Rais Samia kaingia Madarakani, Hakuna Mtanzania Aliyeshtakiwa kwa maoni ya mtandaoni

537 watched
0
3
Published 28 Jun 2021

Deodatus Balile, Mwenyekiti - Jukwaa la Wahariri Tangu ulivyoingia madarakani hakuna redio iliyofungiwa, gazeti lililofungiwa, mtandao au akaunti iliyofungiwa wala Mtanzania aliyefikishwa mahakamani kutokana na kutoa maoni mtandaoni. Tunakushukuru sana. Tuna changamoto nyingi. Kwa uchache sana naomba nipitie mambo ya msingi ambayo yanaathiri vyombo vya habari ambayo naamini yote yanatugusa. Hali ya Uchumi wa Vyombo vya Habari Kuna baadhi ya magazeti na redio ambayo yameamua kujifunga wenyewe kutokana na uchumi ambao ni mbaya sana kwa vyombo vya habari kwa miaka 6 iliyopita. Na hii ni pamoja na magazeti ya Habari Corporation kujifunga na kushindwa kujiendesha. Kulikuwepo kanuni ya kimyakimya kuwa vyombo vya habari vya binafsi visipewe matangazo na matokeo yake serikali ndiyo mtangazaji mkuu, vimeishia kufa kifo cha asili. Bahati mbaya hata wale waliopata matangazo, bahati mbaya hayalipwi kwa wakati. Tunaomba kumshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa alipokuja Morogoro kufungua Mkutano wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Mei 20, alituambia tukusanye hayo madeni yote na tuyapeleke ofisini kwake. Tumeyakusanya; jumla kampuni 8 zimewasilisha madeni na deni lipo kati ya Shilingi Bilioni 6.5 hadi Bilioni 6.8 Waziri Mkuu alisema angeangalia namna kufikia Juni 30 deni hili liwe limelipwa. Mh. Rais, tunaomba uongezee nguvu uamuzi hu una nia njema ya Waziri Mkuu tuone kama tunaweza kuvikomboa vyombo vya habari, maana vinakufa kifo cha asili. Tunaomba utusaidie kufuta hii kanuni ya kimyakimya ya kuvinyima matangazo vyombo vya habari binafsi Tunaomba urejeshe utaratibu wa Serikali kutangaza na vyombo vya habari bila kujali ni binafsi au serikali. Kwa nchi za wenzetu wameangalia hali za waandishi wa habari na vyombo vyao na wakaweka ka-stimulus package ili kuvipa ruzuku ya kuvirejeshea uhai ambavyo vinakufa. Ikikupendeza Mh. Rais, uliangalie hilo kwa hapa Tanzania.

Category

Show more

Comments - 0