Duration 1:53

TAZAMA | BAADA YA AGIZO LA WAZIRI SIMBACHAWENE, POLISI DAR KUANZA KUMUHOJI ASKOFU MWINGIRA

5 198 watched
0
8
Published 27 Dec 2021

Jeshi la Polisi kanda Maalumu ya Dar es salaam limeagiza ndani ya saa 24 kuanza kuhojiwa kwa Askofu wa kanisa la Efatha Josephat Elias Mwingira juu ya tuhuma mbalimbali alizozitoa dhidi ya Serikali ikiwemo njama za Maofisa wa Serikali kutaka kumuua. Jeshi la Polisi limefikia hatua hiyo baada ya kufuatilia kwa karibu kauli zinazodaiwa kutolewa na Askofu huyo na kuona kuwa zinajenga hofu na chuki kwa wananchi dhidi ya Serikali yao. Kwa uzito wa mambo yanayodaiwa kutolewa na Askofu huyo ni lazima apatikane haraka iwezekananavyo na ahojiwe kwa kina juu ya kila kipengele ambacho Jeshi linaona kuna viashiria vya vigezo vya kijinai. Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam linatoa tahadhari kuwa halita sita kumkamata na kumuhoji mtu yeyote ambaye anatumia vibaya Uhuru wa maoni ya kikatiba, na kuwakumbusha wananchi kuwa uhuru huo lazima uzingatie Sheria za Nchi na usikiuke haki na uhuru uliowekwa kwa mujibu wa Sheria. Follow us on: FACEBOOK; SpotiLeo: https://www.facebook.com/Spotileo-176 ... HabariLeo: https://www.facebook.com/habarileo/ DailyNews: https://www.facebook.com/dailynewstz/ INSTAGRAM; HabariLeo: https://instagram.com/habarileo_tz?ig ... SpotiLeo: https://instagram.com/spotileo?igshid ... TWITTER; Twitter HabariLeo: https://twitter.com/HabariLeo?s=09

Category

Show more

Comments - 8